Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala za mtandano huu, ni matumaini yangu kuwa hu mzima na unaendelea vizuri sana katika ile hali ya kupambana ili tu kujiletea mafanikio kwa kiwango kikubwa na unachokihitaji nami nakusihii usichoke kupambana maana mapambano yanaendelea na hakuna haja ya kuchoka wakati mapambano bado yanaendelea.
Wakati unaendelea kupambana ni vyema ukafahamu kuwa katika maisha kuna vitu ambavyo unaweza kuwa unavifanya alafu vitu hivyo vikasababisha wewe ukawa umebakia katika kifungo cha maisha, nadhani kila mtu anaufahamu mnyororo ndio maana siamini kama mtu atapata shida kunielewa naposema ivunje minyororo hii mitatu. Kwa kawaida binadamu huwa tunakuwa katika vifungo vya namna mbalimbali na katika vifungo hivyo huwa tunakuwa
tumefungwa na minyororo mingi sana, na kuikata minyororo hii huwa ni ngumu, hii ni kutokana na sababu kuwa minyororo hii huwa ni migumu kukatika kama ilivyo kiuhalisia kuwa minyororo sio kitu cha kukatika kiurahisi, pili ni sisi wenyewe ambavyo tunafikiri juu ya minyororo hiyo. Nadhani mpaka hapo ndugu msomaji tupo wote kwa asilimia kubwa, sasa twende turudi katika kuitazama minyororo hiyo mitatu ambayo leo nataka uende kuivunja.
tumefungwa na minyororo mingi sana, na kuikata minyororo hii huwa ni ngumu, hii ni kutokana na sababu kuwa minyororo hii huwa ni migumu kukatika kama ilivyo kiuhalisia kuwa minyororo sio kitu cha kukatika kiurahisi, pili ni sisi wenyewe ambavyo tunafikiri juu ya minyororo hiyo. Nadhani mpaka hapo ndugu msomaji tupo wote kwa asilimia kubwa, sasa twende turudi katika kuitazama minyororo hiyo mitatu ambayo leo nataka uende kuivunja.
1. Mafunzo mabovu ya dini, awali ya yote ningependa kusema sipo hapa kuwakosoa waubiri au kusema kuwa wanatoa mafunzo ya uongo kwa watu hapana bali hapa nipo katika kueleza uhalisia wa mambo. Kwa jamii nyingi sana za kitanzania mtu anapokuwa mtoto mdogo huwa anasissitizwa sana katika maswala la dini hii ni pamoja na kuwalazimisha watoto kwenda kanisani na kuweza kupata mafunzo mbalimbali ya kidini. Sasa hapa katika dini tunaweza tukapata mafunzo mbalimbali ambayo muda mwingine huwa minyororo kwetu ambayo inatutia katika kifungo. Mfano watoa mafunzo wengi sana wamekuwa na mtazamo hasi juu ya pesa wengi wamekuwa wakiamini kuwa pesa ni chanzo cha uovu na kuwakanya sana wafuasi wao juu ya kupenda pesa. Hiki sasa ndicho kifungo, ukiamini kuwa pesa ni chanzo cha maovu kutokana na mafunzo uliyopewa huko kanisani unakuwa katika wakati mgumu sana katika utafutaji wa pesa na hivyo unaweza kujikuta hauzipati pesa hizo hii ni kutokana na mtazamo wako juu ya pesa. Pesa sio chanzo cha maovu maana pesa haina uamuzi juu ya binadamu.
2. Saikolojia mbovu, saikolojia ni sayansi inayohusiana na tabia ya mwanadamu. Hapa katika saikolojia tunaangalia jinsi gani mazingira ya mtu fulani toka utotoni mwake mpaka anavyokuwa mtu mzima yanavyoweza kumwathiri mtu husika. Mfano kama toka ukiwa mtoto mdogo wazazi wako na ndugu zako walikuwa hawana imani na wewe na wamekuwa wakisema wewe huwezi lolote maishani utakuwa huku ukiwa umejengeka na fikira hizo mpaka unakuwa mtu mzima. Kutokana na hili unaweza kuja kuteseka sana katika utu uzima wako kwani utakuwa ni mwenye kuamini kuwa hauwezi lolote hii ni kutokana na yale maneno ya wazazi na ndugu juu yako. Sasa leo ni siku ya kujiondoa katika kifungo hicho kwa kukata minyororo hiyo ya saikolojia mbovu ambayo walikujengea huko nyuma.
3. Mipango mibovu, ulishawahi waza juu ya mipango yako?, je unajua kuwa wakati mwingine unaweza kuwa haufanikiwi katika jambo fulani kutokana na mipango yako mibovu unayojiwekea. Katika maisha usiwe mtu wa kuweka mipango bora umeweka bali kuwa mtu mwenye kuweka mipango mathubuti, mipango bora ambayo inaweza kukusukuma wewe na kuweza kukufanya uweze kusonga mbele zaidi na zaidi. Sio unakuwa mtu wa kuweka mipango hata isiyoeleweka alafu unaikomalia kweli.
Nimekuwekea minyororo hiyo mitatu nikiwa na imani kuwa utakwenda kuivunja leo bila kujali hali yako. Kama utashindwa kuivunja maana yake bado utaendelea kuishi kitumwa au kifungwa na usipoangalia unaweza kuwa mfungwa wa jumla mpaka mwisho wa maisha yako.
“yakale hayana nafasi sasa, usijilaumu juu ya yale yaliyotokea kale maana hayo yamepita. Unaweza kuanza upya leo, usijione nikama umechelewa kwani wakati bado”

No comments:
Post a Comment